Zikiwa zimepita siku chache tangu Shirika la Posta lianze kutoa huduma ya kusafirisha abiria na vipeto kwa njia ya mabasi, waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kusimamia biashara hiyo kwa kufuata maadili.
Wito huo ulitolewa na Profesa Mbarawa alipokuwa akifungua Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Posta jijini Dar es Salaam juzi.
Profesa Mbarawa alisema kwa muda mrefu, mali zake na miradi ya shirika hilo imekuwa ikiwanufaisha wachache wasiokuwa na maadili na kwamba, uongozi wa awamu hii hautafumbia macho vitendo hivyo ikiwamo mradi wa mabasi.
Katika hatua nyingine, waziri huyo aliwashauri wafanyakazi hao kuchagua viongozi wasioendekeza siasa ofisini, hivyo kuathiri shughuli za shirika.
“Kuna baadhi ya viongozi wao tangu wanaingia madarakani ni kuendekeza tu siasa, hivyo kuacha kushughulikia maslahi mapana yanayowahusu wafanyakazi. Ndugu zangu watu wa aina hii msithubutu kuwachagua kwani hawatawafikisha popote zaidi ya kuleta malumbano yasiyo na tija kwenu,” alionya waziri huyo.
Awali, mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Dk Harun Kondo alisema licha ya malengo mazuri waliyojiwekea wafanyakazi, zipo changamoto mbalimbali zinazoendelea kulikabili shirika hilo ikiwamo suala la madeni wanayoyadai mashirika na taasisi za Serikali.
Dk Kondo alisema deni hilo linalofikia Sh4 bilioni ambalo linawafanya kushindwa kusukuma baadhi ya mambo ya maendeleo, hivyo kumuomba waziri kuwasaidia katika kukumbusha ili walipwe na kuweza kutekeleza majukumu yao kama walivyojipangia.
“Kwa mfano tumebebeshwa mzigo wa kuwalipa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki jambo ambalo halikuwa sahihi, hivyo fedha zilizotumika kufanya jambo hilo ni vyema zikarudishwa,” alisema mwenyekiti huyo.
Malipo ya wafanyakazi EAC
Kwa mujibu wa taarifa ya aliyekuwa waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo aliyoitoa bungeni Novemba 5, 2008, wafanyakazi wa Posta 1,041 wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)walilipwa Sh4.3 bilioni.