Mwanariadha Giniki azidi kuchanja mbuga kimataifa

Mwanariadha Emmanuel Giniki amezidi kujitangaza kimataifa na kupata mashabiki zaidi kutokana na kufanya vyema kwenye mialiko yake na sasa amejitokeza mdau akitaka kuinunu jezi yake kwa gharama yoyote.

Giniki alisema tukio hilo limetokeza nchini Hispania alipokwenda kushiriki mashindano ya xxxvi Cross Internacional de Ita’lica ya 10 km aliyomaliza nafasi ya tano akitumia wa dakika 31:08 wa kwanza akiwa Joshua Cheptegei wa Uganda aliyetumia dakika 30:54.

“Nlipomaliza alitokea Mzungu aliniomba mazungumzo na mimi, lakini nikamjibu asubili kuna vitu namalizia kisha tutaongea vizuri ambapo akaomba mawasiliano yangu na sikujua anataka nini kwangu,” alisema Giniki.

“Nikiwa safarini nikaona ujumbe kutoka kwake akijitambulisha kuwa anaitwa Juan Nigreira ambaye ni profesa na mhadhili katika moja ya chuo Kikuu nchini Sweden na mmoja ya wafuatiliaji wa wanariadha wa Tanzania kwa muda mrefu hivyo anaomba kununua jezi yangu nikamjibu asubuli hadi ninapopata ruhusa ya shirikisho.”
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items