Rais John Magufuli akitia saini katika kitambo cha maomboleza ya kifo cha Jaji Mstaafu, Robert Kisanga.
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi leo ameongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam kuuga mwili wa Jaji Mstaafu Robert Kisanga aliyefariki mwanzoni mwa wiki hii.
Kabudi ameongoza mamia ya wakazi hao walioaga mwili ya Kisanga katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Msasani.
Viongozi wengine walioshiriki kuuaga mwili huo ni pamoja ni Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, Mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Anna Mkapa na Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, majaji na viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali.
Kwa mujibu wa mjukuu wa marehemu, Fred Kisanga amesema mwili wa marehemu utazikwa katika kijiji cha Mbokomu, Mkoa wa Kilimanjaro
