Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas Serikali kushusha treni mpya za umeme amesema uchumi wa wetu umekua kwa kasi ambapo kwa Nchi za Afrika, Tanzania inakamata namba tank.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imezitaja nchi 10 ambazo uchumi wake utakua kwa mwaka huu huku Tanzania ikiwa ni miongoni mwa Nchi hizo.
Dk Abbas pia amezungumzia suala la kuhamia mjini Dodoma kama ambavyo Serikali ilitangaza hapo awali ambapo tayari wafanyakazi 3600 wameshahamia katika mji huo ambao ni makao makuu ya Nchi.
" Nitumie fursa hii kuwaeleza watu kwamba Serikali imeshahamia Dodoma, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais pia wameshahamia., na mwaka huu wafanyakazi 2060 watahamia.
" Kwa wale ambao walikua hawaamini sasa nawashauri waende Dodoma kuchukua fursa zilizopo, Mheshimiwa Rais na yeye yupo mbioni kuhamia huko, kwahiyo Dodoma kuchele," Alisema Dk Abbas.
Kuhusu ukuaji wa Viwanda alisema hadi kufikia robo ya mwaka jana viwanda zaidi ya 3000 vimeshajengwa na 600 kati ya hivyo ni viwanda vikubwa huku akitolewa mfano kiwanda cha Sayona na kiwanda cha kuunganisha matrekta.
" Tunaposema hizi takwimu za viwanda siyo nadharia tena ni vitendo ndio maana katika viwanda vyote hivyo vimeajiri zaidi ya wafanyakazi 50000, hivyo tunavyosema Tanzania ya viwanda kila Mtanzania anaweza kuwa nacho," Alisema Dk Abbas.
Dk Abbas alisema ili Tanzania ya viwanda ifanikiwe inahitaji nishati ambapo alizungumzia miradi ya umeme Kinyerezi II ambapo mpaka sasa megawati 240 zimekamilika kwa asilimia 80, huku mradi wa Kinyerezi I megawati 185 zikiwa zimekamilika kwa
asilimia 50.
Kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge, Dk Abbas alisema kuna vipande vya Kilomita 300 kutoka Dar e Salaam ambacho tayari kimeshaanza kufanyiwa kazi ambapo wataalamu wa ndani na nje ya Nchi wapo kazini usiku na mchana kuhakikisha ujenzi huo unaanza.
" Sisi kama Serikali hatusubiri hadi reli ikamilike ndo tutafute treni, tumeshaanz mchakato wa kununua treni za kisasa za umeme na za kawaida ambazo zinatumia Diesel.na tayari zabuni imeshatangazwa na itafunguliwa mwishoni mwa mwezi huu.
" Tunanunua mabehewa ya kisasa 1590 ambazo treni moja itakua na uwezo wa kubeba kontena 100, lakini pia mabehewa yenye makochi ya kisasa lakini pia vichwa 25 vya treni," Alisema Dk Abbas.
Kuhusu usafiri wa majini, Serikali imesema imehakikisha inaboresha ambapo meli mpya ya kisasa itapelekwa Ziwa Nyasa lengo ni kuifanya Tanzania kuimarika zaidi kiuchumi.