Watoto 500 wa mitaani waanzishwa elimu ya msingi

Wilaya ya kiteto imefanikiwa kuwakamata zaidi ya watoto 500 kutoka jamii ya wafugaji ambao wazazi wao hawakuona umuhimu wa kuwapeleka shule ambao sasa imewakusanya kwenye shule za msingi za bweni wilayani humo kwa ajili ya kuanza kusoma huku ikitarajia kufikisha watoto 1000 ndani ya mwaka huu kutokana na wingi wao kuwa mitaani.

Kiteto imekuwa na wimbi kubwa la watoto wasiokwenda shule hivyo kuilazimu serikali kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya kufanya operation ya kuwakamata na kuwapeleka shule watoto ambao hawajaanza masomo licha ya kufikia umri wa kuanza shule.

Ngayeni Ngoroi ni mmoja ya watoto ambao kwa sasa hajawahi kuandikishwa shule licha ya kuwa na umri zaidi ya miaka 10 lakini ili Ngayeni aweze kupata haki hiyo ya msingi ameamua kujitoa mhanga na kutoroka nyumbani hadi shule ya Partimbo ambayo ni zaidi ya kilomita 100 kutoka eneo la lesoit nyumbani kwao na hapa anaeleza kwanini hajaanza shule na umri huo.

Kutokana na kilio hicho cha shule ya msingi Partimbo ya chakula mkuu wa mkoa wa Manyara ameahidi kutoa shilingi milioni 1 kwaajili hiyo lakini serikali haiachi kuwanyooshea kidole wazazi jamii ya wafugaji pamoja na wakulima wa kuhamahama juu kupeleka watoto shule.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items