Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka vijana wa timu ya Serengeti Boys wenye umri wa miaka 16, kupambana kwa hali na mali ili waweze kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Dkt. Mwakyembe amesema hayo wakati akiwasilisha salamu za serikali pindi alipokuwa amewatembelea vijana katika kambi yao waliyoiweka katika hostel za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jijini Dar es Salaam leo (Jumamosi).
"Pambaneni kwa ajili ya Tanzania na hakikisheni mnafanya vyema kwenye kila mashindano na makocha wa kikosi hakikisheni mnawapa mafunzo mazuri kwa ustawi wa vijana. Naamini mtaimarika na kuwa bora maana hata TFF hii sasa ina ari na morali kubwa", alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha Dkt. Mwakyembe amesema anaamini vijana hao watakuwa bora chini ya TFF iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais Wallace Karia.
Kwa upande mwingine Dkt. Mwakyembe alipata nafasi ya kutazama mchezo wa kirafiki kati ya Serengeti Boys dhidi ya Makongo Sekondari ambao ulimalizika kwa Serengeti kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Kabla ya mchezo huo Serengeti Boys walicheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Kituo cha Bombom iliyomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.