Mshambuliaji Mbelgiji, Michy Batshuayi anayecheza kwa mkopo kutoka Chelsea akibinuka sarakasi baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 49 katika ushindi wa 2-0 wa Borusia Dortmund dhidi ya Hamburg kwenye mchezo wa Bundesliga usiku wa jana Uwanja wa Signal-Iduna-Park. Bao la pili la Borusia Dortmund lilifungwa na Mario Gotze dakika ya 90 na ushei.
