Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Halmashauri ya Jiji la Arusha imeanza mchakato wa
kuwasilishi mapendekezo ya bajeti mpya
ya mwaka 2018/19 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 6.9 zitatengwa kwa ajili ya
kutekeleza miradi mbalimbali ya kuwaudumia wananchi hususan katika sekta ya
afya,elimu na miundombinu ya barabara.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Athumani Kihamia amesema kuwa
tayari wameanza kukaa vikao vya mapendekezo ya bajeti na Watendaji wa
Kata,Viongozi wa Dini,Makundi ya Wazee na Vijana ili kupata maoni yao juu ya
vipaumbele vya bajeti hiyo ili iweze kutatua changamoto ya wananchi iwapo
itatekelezwa kama ilivyopangwa.
Kihamia aliyasema hayo wakati akizungumza katika kikao cha
mapendekezo ya bajeti kilichofanyika katika ukumbi ulioko katika Ofisi za Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,ambacho kilihudhuriwa na wadau mbalimbali.
Baadhi ya wajumbe wamependekeza kuwekwa kipaumbele katika
suala la ujenzi wa madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani
jambo ambalo litasaidia kuboresha maendeleo ya taaluma mashuleni.
Kufuatia Ongezeko la Ufaulu wa Wanafunzi wanaojiunga na
kidato cha kwanza ,MKuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro ameitaka
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuhakikisha wanajenga madarasa ya kutosha ili
kuepusha msongamano na uhaba wa vyumba vya madarasa katika kipindi cha mwanzoni
mwa mwaka ambacho wanafunzi wengi hujiunga na masomo ya sekondari.
Akizungumza katika kikao cha Mapendekezo ya bajeti ya mwaka
2018/19 ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali
wa maendeleo wakiwemo Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata 25 zilizoko jiji la
Arusha ,Daqqaro amesema kuwa watendaji wa serikali wanapaswa kuachana na tabia
ya kuwajibika pindi wanapoona wanafunzi wamekosa madarasa na badala yake
watenge fedha za kujenga madarasa mapema .
Naibu Meya wa Jiji la Arusha Viola Lazaro alisema kuwa hulka
ya baadhi ya watendaji kushughulikia
tatizo la uhaba wa madarasa kipindi ambacho kina idadi kubwa ya wanafunzi
wanaojiunga na sekondari imekua
ikiwagharimu watoto kushindwa kufanya vizuri kitaaluma kutokana na msongamano
wa wanafunzi Tito Cholobi
Afisa Tarafa Elerai alisema kuwa ni vyema serikali ikatenga fedha
kwa ajili ya kujenga madarasa ya kutosha angalau madarasa 160 kwa kila mwaka
ili kuziba pengo la uhaba wa madarasa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Athumani Kihamia
amesema kuwa serikali itajitaidi kuhakikisha kuwa inajenga madarasa ya kutosha
kwani ni kipaumbele cha serikali kuboresha elimu na taaluma kwa ujumla.
