Na Omary Mngindo, Kibiti Rufiji
SERIKALI wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani, Tanzania imetenga kiasi cha sh. Bil 5. 3 kwa ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya hiyo yanayojengwa na SUMA JKT ambayo kwa sasa upo hatua ya kuchimba msingi.
Aidha katika mwaka huu wa fedha imetenga sh. Bil. 2.4 kwa ujenzi wa daraja kubwa la kuunganisha eneo la Mbuchi na Mbwera lenye urefu wa mita kumi, kazi inayoendelea pamoja na daraja la Mwake lenye urefu wa mita 40 kwa thamani ya sh. Mil. 969.1.
Taarifa iliyomwa na Makamu Mwenyekiti Yusuph Mbinda mbele ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno, imeeleza kuwa sanjali na hilo wakandarasi wanafanya utafiti wa vyanzo vya uchimbaji visima katika vijiji mbalimbali lengo kuwaondolea kero hiyo wananchi.
"Vijiji vinavyotaraji kunufaika na mpango huo ni pamoja na Nyamisati, Mtunda, Mchungu, Mahege, Kivinja A, Ruma, Mlanzi, Mjawa, Nyakinyo, Kilula, Tambwe, Bumba Msoro na Miwaga/Ngulakula mradi unaogharimu sh. Mil. 319.2.
Imefafanua kwamba kupitia utekelezaji huo unaosimamiwa na ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, baada ya kukamilika kwa mradi huo utaoendana na upatikanaji wa maji, utaongeza idadi ya watumiaji huduma hiyo kutoka 24,581 sawa na asilimia 65 mpaka kufikia 122,648 sawa na asilimia 85.
Ikizungumzia suala la chakula, taarifa hiyo ya Mbinda imeeleza kwamba hali ni nzuri, na kwamba hiyo inatokana na wananchi kujikita zaidi katika kilimo cha kisasa cha mazao ya chakula sanjali na ya biashara yakiwemo ya mpunga, mahindi, ufuta, muhogo na korosho.
"Pamoja na chanagmoto ya soko la zao kuu la biashara, upande wa korosho kutokana na ubora wake, bado tunaimani kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi tutaweza kuwasaidia wananchi wetu kujikwamua kupitia kilimo hicho," ilieleza sehemu ya taarifa.
Imeongeza kwamba kwa mwaka wa 2017/2018 Kibiti pekee imezalisha tani 5,430,667 kutoka tani 3,713,163 mwaka 2016 sawa na ongezeko la asilimia 46.25 ya uzalishaji wa zao hilo.
Ikizungumzia mifugo, taarifa hiyo imeeleza kuwa wilaya inakadiliwa kuwa na ng'ombe 44,739, mbuzi 5,368 na kondoo 3,517 huku vijiji 19 kati ya 58 vimetenga maeneo ya malisho baada ya mpango wa matumizi bora ya ardhi, jumla ya hekta 21,984.79 zimetengwa kwa ajili ya malisho huku zoezi la upigaji chapa mifugo likiendelea.