Mabalozi wa mataifa kumi-na-moja, wakiwemo wa Marekani na Uingereza nchini Kenya, wamemtaka kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Bwana. Raila Odinga kumtambua Rais Uhuru Kenyatta kuwa ni Rais halali aliyechaguliwa.
Katika taarifa ya pamoja ya mabalozi hao wamesema Bwana Odinga hanabudi kumtambua Rais Kenyatta kuwa ni Rais ikiwa ni msingi wa mazungumzo ambayo wananchi wengi wa Kenya wanayataka yafanyike.
Wiki iliyopita kiongozi wa upinzani Bwana. Raila Odinga alijiapisha kuwa Rais wa wananchi na Serikali kwa upande wake iliwakamata baadhi ya watu walioshiriki kwenye hafla hiyo na kuvifunga baadhi ya vituo vya televisheni vilivyoonesha tukio hilo.