Mashambulizi yaliyofanywa na Israel yaungwa mkono na Marekani

Marekani imeunga mkono mashambulizi yaliyofanwa na Israel na kusema ni vizuri kuwa Israel imeweza kuilinda mipaka yake.

Hii ni baada ya jeshi la Israel kuishambulia "drone" ya Iran iliyokuwa imerushwa kutoka Syria.

Msemaji Heather Nauert ameionya Iran kuacha matendo ya kuhatarisha amani.

Heather amesema kuwa Washington ipo bega kwa bega na Israel katika kuilinda mipaka yake dhidi ya wanajeshi wa Syria kusini wanaosaidiwa na Iran.

Hata hivyo Iran imekana madai ya Israel kuhusu kurusha ndege isiyokuwa na rubani mpakani mwa Israel.

Mpya zaidi Nzee zaidi