Urusi: Ndege yenye abiria 71 yaanguka ikipaa

Ndege ya Urusi iliyokuwa imebeba abiria 71 na mhudumu imeanguka baada ya kupoteza mawasiliano ilipokuwa ikiondoka uwanja wa mjini moscow.

Ndege hiyo ya shirika la Saratov ya An-148, ilikuwa safarini kwenda mji wa Orsk wakati ilipoteza mawasiliano.

Huduma za dharura ziliambia vyombo vya habari kuwa ndege hiyo ilianguka na hakuna uwezekano wa kuwapata manusura,

Inaripotiwa kuanguka karibu na Argunovo kilomita 80 kusini mashariki mwa Moscow.

Kulingana na shirika lingine na habari ndege hiyo ilipotea kutoka mitambo ya rada dakika mbili baada ya kuondoka uwanja wa Domodedovo.
Mpya zaidi Nzee zaidi