Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Dk. Ainea Mlewa, alisema kwamba matukio yote yalitokea mapema wiki hii katika Kitongoji cha Waraka, Kijiji cha Lusilile, tarafa ya Kintinku.
Dk. Mlewa aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Victoria Samweli (50), Matembe Samweli (8) na Mosi Samweli (11) wote wakazi wa Kijiji cha Lusilile.
Alisema katika tukio la kwanza walipokea watu wawili wa familia moja waliokuwa na hali mbaya kutokana na kula chakula kinachosaidikiwa kuwa na sumu wakati mtoto mmoja alipoteza maisha wakiwa njiani kabla ya kufikishwa hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa Dk. Mlewa, wagonjwa hao wawili waliofikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni walipoteza maisha wakati wakipatiwa matibabu.
Dk. Mlewa alisema katika tukio lingine mama aliyejulikana kwa jina la Christina Boniphace (43) mkazi wa Kitongoji cha Waraka, Kijiji cha Lusilile alifariki dunia baada ya kukatwa panga na kaka yake walipokuwa wakitoka kwenye sherehe za kimila, maarufu kwa jina la kunywa mchuzi.
Alisema walipofika njiani kaka yake alimvuta dada yake mafichoni na kuanza kumkatakata kwa panga hali iliyosababisha kufikishwa katika Hospitali hiyo lakini juhudi za kuokoa maisha yake hazikuzaa matunda.
Mtoto wa marehemu Christina aliyekatwa panga na kaka yake, Fredrick Stephano, alisema taarifa za awali alizopata kuhusiana na tukio hilo zilibainisha kwamba mama yake na mjomba wake hawakuwa na ugomvi wowote, bali walitofautiana kauli baada ya mama yake kumjibu kaka yake huyo kuwa walikokuwa wakienda ni nyumbani, jibu ambalo kaka yake hakuridhika nalo na ndipo alitoa panga na kumkata.
Gasper Mgante, Diwani wa Kata ya Kintiku, akizungumzia tukio hilo, alisema limetokea saa saba usiku wakati wakirudi nyumbani.