Umoja wa Mataifa umesema takriban watu 47 wakiwemo wanawake na watoto wameuawa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Watu hao waliuawa katika msako wa serikali dhidi ya waandamanaji wanaomtaka Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila kuachia madaraka.
Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kati ya tarehe 1 Januari mwaka jana na tarehe 31 Januari mwaka huu, watu wasiopungua 47 waliuawa na maafisa wa usalama wakati wa maandamano na kuongeza kuwa kulikuwa na jaribio la vyombo vya dola kufunika ukweli kuhusu vifo hivyo kwa kuiondoa miili ya waathiriwa na kuhujumu uchunguzi wa waangalizi wa Congo na wa kimataifa.
Ripoti hiyo imesema ili kuwepo uchaguzi huru na wa kuaminika tarehe 23 mwezi Desemba serikali ina wajibu wa kuhakikisha haki za kiraia na kisiasa zinaheshimiwa.