Rais Zimbabwe achapisha mamia ya watu walioshindwa kurejesha fedha za serikali

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amechapisha mamia ya majina ya watu na makampuni ambayo yameshindwa kurejesha kiasi cha dola za Marekani milioni 827 ambazo wamezihifhadhi nje ya nchi hiyo kinyume cha sheria.

Baada ya kuchukua madaraka kama rais mwaka uliopita, rais Mnangagwa alitoa muda wa siku 90 kwa watu na makampuni kurejesha kiasi hicho cha fedha kwa kubadilishana na msamaha.

Rais Mnangagwa amesema agizo lake limesababisha kurejeshwa kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 591 ikiwa ni chini ya nusu ya kiasi kinachodhaniwa kuwa kimefichwa nje ya nchi hiyo.

Aidha Rais huyo kwenye taarifa yake aliyoitoa juma hili amesema wale walioshindwa kurejesha ndani ya muda aliokuwa ameutoa watakabiliwa na mkono wa sheria.
Mpya zaidi Nzee zaidi