Uingereza na Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano ya kihistoria ya awamu ya mpito ambayo itadumu kwa karibu miaka miwili baada ya kutimizwa hatua ya kihistoria ya Uingereza kujiondoa katika umoja huo mwaka ujao.
Pande hizo mbili pia zimefikia muafaka kuhusu suala nyeti la mustakabali wa mpaka wa Ireland, wiki chache tu baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, kusema hakuna waziri mkuu yeyote wa Uingereza angeweza kukubali wazo la aina hiyo.
Kiongozi wa mazungumzo ya Umoja wa Ulaya kuhusu Brexit, Michel Barnier, amesema kipindi cha mpito kitaanza mnamo siku ambayo Uingereza itajiondoa rasmi – ambayo ni Machi 29 mwaka wa 2019 – na kudumu hadi Desemba 31, 2020.