Kundi la Jama Nusrat Ul Islam wa Al ladai kuhusika na shambulio la Burkina Faso

Viongozi wa Burkina Faso wamewahimiza watu nchini humo kuwa waangalifu baada ya mashambulizi ya kigaidi kuyalenga makao makuu ya jeshi na ubalozi wa Ufaransa nchini humo siku ya Ijumaa ambapo watu wanane waliuawa.

Kundi la wanamgambo wenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda kutoka nchi jirani ya Mali limedai kuhusika na mashambulizi hayo.

Mashambulizi hayo ni ya tatu kufanyika Burkina Faso katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na mara hii kuyalenga makao makuu ya jeshi na ubalozi wa Ufaransa kumeibua wasiwasi kuwa wanamgambo wa Afrika Magharibi wanazidi kupata makali ya kufanya mashambulizi makubwa zaidi.

Kundi lijulikanalo Jama Nusrat Ul Islam wa Al Muslimin limesema lilifanya mashambulizi hayo kulipiza kisasi kuuawa kwa mmoja wa viongozi wake na wanajeshi wa Ufaransa
Mpya zaidi Nzee zaidi