Wafanyakazi wa kutoa misaada wauawa na Boko Haram

Wafanyakazi watatu wa kutoa misaada wameuawa katika shambulizi lililofanywa na kundi la Boko Haram katika mkoa wa Rann ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Samantha Newport amesema, mfanyakazi wa nne anashukiwa kuuliwa na mwingine kutekwa nyara katika shambulizi hilo.

Wafanyakazi wote ni raia wa Nigeria.
Mpya zaidi Nzee zaidi