Nuh Mziwanda awajibu watu kwa vitendo wanaodai amefulia


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Nuh Mziwanda ameonekana kukerwa na baadhi ya maoni ya watanzania wanadai kuwa msanii huyo kwa sasa kafulia tangu wamwagane na aliyekuwa mpenzi wake, Shilole.

Nuh amewajibu watu hao wanaomuandamana kwa kuwaonesha mjengo wake mpya ambao upo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam maeneo ya Kivule na kuandika maneno ambayo bila shaka ni jibu tosha kwa watu hao.

Mjengo mpya wa Nuh Mziwanda ambao bado haujakamilika

“Mjini wengi wajanja wao ‘Sisi Wajinga Daily hatuna Mipango ila kila Mafanikio yapo Moyoni Mwa Mtu acha tuendelee kuchorana tu. Hii hapa ya Mwanangu Anya Kwa Nguvu za Mungu imefikia Hapo Kivule Moja. Endeleeni Kumzungumzia Nuh halafu Mie nafanya Wonders.“ameandika Nuh Mziwanda kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwa upande mwingine, Nuh Mziwanda amesema kuwa mashabiki wake wakae tayari kwa ujio wa lebo yake mpya ya muziki ya Last Born Records.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia