Mkuu wa wilaya ya Kilwa agawa namba simu kwa wanafunzi ili kupambana na Mimba

Na.Ahmad Mmow,Lindi.
BAADA ya kusikia malalamiko ya wazazi na walezi wa kata ya Mingumbi wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi. Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai amegawa namba za laini za simu zake kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya Migumbi ikiwa ni sehemu ya kudhibiti tatizo la mimba kwa wanafunzi.

Hayo yalimejiri leo katika kijiji cha Mingumbi wakati mkuu huyo wa wilaya alipozungumza na wazazi,walevcc
zi,wajumbe wa bodi na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Mingumbi.

Ngubiagai alifikia kugawa namba hizo za simu baada ya kuzungumza na kusikia malalamiko kutoka kwa wazazi na walezi sababu za wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kupata ujauzito.

Baada ya mkuu huyo wa wilaya kutoa nafasi kwa wananchi,walezi na wazazi kutoa maoni yao kuhusu tatizo hilo.

"Nimelazimika kuwapa namba za simu ili wakati wowote kukiwa na walimu au watumishi wa umma wengine wataowanyemelea na kuanza kuwalaghai mfanye nao mapenzi nijulisheni haraka.

Niambieni majina yake,anaishi wapi na anafanya kazi gani. Mimi nitahangaka nao,nimeishi katika wilaya nilizoongoza kabla ya kuhamia wilaya hii sikuwahi kuona wala kusikia mwalimu wa kike anawatongoza wanafunzi wa kike nawakabidhi wanaume, lakini hapa Kilwa imeanza tabia hiyo, "alisema Ngubiagai.

Kabla ya kuzungumza na wanafunzi, Ngubiagai akizungumza na wazazi, walezi, wajumbe wa bodi ya shule na walimu,alisema hatokubali kuona walimu na watumishi wa umma wilayani humo kuwa sehemu ya tatizo hilo.Huku akiwataka wazazi kuwafichua watumishi wenye tabia hiyo na kuacha kumalizana na watenda uovu nje ya mahakama.

"Leo mwalimu wa kike anakamatwa kujihusisha na vitendo vya kuwarubuni watoto wa kike wafanye mapenzi na wanaume. 

Halafu wanakamatwa na ushahidi upo nasikia kuwa wapo nje kwa dhamana na kwamba suala hilo limekwenda kwa mkurugenzi wa mashitaka, sijui katika kipindi hiki wazazi wa mwanafunzi huyo watajikiaje, huyo mwanafunzi atakuwa katika mazingira gani na vipi kama ushahidi hautuvurugwa,kwakweli nashangaa tu, "Ngubiagai alilalamika bila kueleza kisa halisi kinagaubaga.

Mkuu huyo wa wilaya wa wilaya alitoa wito kwa mamlaka zinazotoa haki na kutafsri sheria kuharakisha kutoa uamuzi kuhusu mashauri yanayohusu mimba. Huku akiviasa vyombo vya dola kufikisha mahakamani kesi za aina hiyo, visiwe sehemu ya kutengeneza urasimu usio na lazima unaosababisha malalamiko.

Awali baadhi ya wazazi na walezi walimueleza mkuu huyo wa wilaya hiyo kwamba baadhi ya walimu na watumishi wa umma wa umma wanawajaza mimba wanafunzi.Hata walimu nawatumishi hao kesi zao hazifiki mbali zinakwisha kienyeji.

Walisema baadhi ya mimba za wanafunzi wanapewa na kusingiziwa vijana wa mitaani.Hali inayowajengea uhasama viongozi na watendaji wa vijiji dhidi ya wazazi wa vijana hao.

Shule ya sekondari ya kutwa ya kata ya Mingumbi nishule ya kwanza katika wilaya ya Kilwa,shule ya saba kwa mkoa wa Lindi katika matokeo ya ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne wa mwaka jana.


Mpya zaidi Nzee zaidi