NGOs zitakazofanya kazi kinyume na sheria kufutiwa usajili

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) imesema haitasita kulifutia usajali Shirika lolote lisilo la Kiserikali litakaloenda kinyume na Sheria na Taratibu za nchi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba alipokuwa akifungua kikao kati yake na Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali na Wadau wa mashirika hayo kwa Mkoa wa Mwanza.

Bw. Katemba amesisitiza kuwa kwa mujibu wa Sheria namba 4 ya Mwaka 2002 ya Mashirika Yasito ya Kiserikali inayataka Mashirika hayo kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Nchi katika utendaji wa kazi zao kwa mujibu wa Katiba na majukumu yao kiusajili.

Ameongeza kuwa kikao hicho kimefanyika ili kuwakumbusha wadau wa NGOs kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria za nchi zilizopo kwani baadhi ya mashirika hayo yamekuwa yakitumika kufanya mambo ambayo yapo kinyume na Sheria.

“Nawataka wamiliki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuzingatia matakwa ya usajili wao katika kutekeleza majukumu katika Mashirika yao” alisema Bw.Katemba
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia