Hiyo ni baada ya operesheni ambazo zimekuwa zikifanywa na jeshi la Uturuki dhidi ya magaidi katika maeneo mbalimbali Syria.
Ripoti zinaonyesha kuwa kwa sasa ni raia 3,567,000 wa Syria wanaishi nchini Uturuki.
Operesheni ya tawi la mzaituni iliazishwa na jeshi la Uturuki mnamo mwezi Jnauari kupigana na magaidi katka mipaka yake na vilevile kuwalinda raia wa Syria.
Wizara ya mambo ya ndani ya Uturuki imeichukulia hatua hiyo kama hatua muhimu katika kurusidha amani nchini Syria.
Wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa wakimbizi kutoka Syria wamekuwa wakihudumiwa kama raia wa Uturuki bila tofauti yoyote.
