Shirika la Afya ulimweguni WHO, leo limezindua kampeni ya kutokomeza homa ya manjano barani Afrika ifikapo mwaka 2026 ijulikanayo kama EYE.
Kampeni hiyo iliyotiwa saini mjini Abuja nchini Nigeria kati ya WHO , shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF pamoja na serikali ya Nigeria imesimamiwa na mkurugenzi mkuu wa WHO Doctor Tedros Adhanom Ghebreyesus, na Profesa Isaac Folorunso ambaye ni waziri wa afya na pia mkuu wa ushirika wa masuala ya afya ukanda wa Afrika magharibi.
Baadhi ya wawakilishi kutoka nchi za Afrika na Amerika Kusini kwenye kampeni hiyo wameelezea matatizo wanayokabiliana nayo katika kutomeza homa ya manjano katika maeneo mbalimbali duniani.
WHO na mashirka wadau wako mstari wa mbele katika juhudi za kuelekeza nguvu zao katika kampeni hiyo ambayo ni moja ya ajenda ya maendeleo enedleevu ya Umoja wa mataifa ya 2030.
Miongoni mwa waliohudhuria kampeni hiyo ni pamoja na UNICEF, mashirika mengine ya kibinadamu, nchi za Afrika Magharibi na GAVI.