Na Ferdinand Shayo, Arusha
Kuna uhusiano mkubwa kati ya mtazamo alionao mtu na aina ya maisha aliyonayo kwasababu maisha yetu ni matokeo ya mitizamo yetu katika Nyanja mbalimbali za maisha, familia, uchumi n.k.
Mtazamo unaanzia na wewe jinsi unavyojiona ,unaona nini ndani yako,unajionaje? Unawaonaje wenzako,unawaonaje waliokuzunguka,familia yako na unaliojae taifa lako na taifa lingine pia.
Maandiko Matakatifu yanaeleza kuwa “Ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo.Swali linabaki kwako unajionaje?
Ukilima na kupalilia vizuri mitazamo yako na kupanda mbegu bora unaweza kubadilisha fikra zako na kubadilisha maisha yako.
Mtu hutenda kile anachofikiria,mtu ni matunda ya fikra zake,tupo hivi tulivyo kwasababu ya fikra na mitazamo yetu.
Ukifikiri vyema utatenda vyema,ukifikiri vibaya utatenda vibaya ndio maana ni muhimu kuwekeza katika mitazamo.
Mabadiliko yanaanzia kwenye mtazamo ,mtazamo ndio kiini ambacho kikibadilika fikra zinabadilika,utendaji unabadilika
Tags:
makala
