Ommy Dimpoz arudishwa Sauzi kutibiwa

STAA wa Bongo Fleva, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amerudishwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu baada ya hali yeke kuendelea kutokuwa vizuri licha kutolewa hospitalini huko siku chache zilizopita.

Dimpoz ambaye miezi miwili iliyopita alifanyiwa upasuaji mkubwa wa koo nchini Afrika Kusini, hali yake imekua haiimariki ipasavyo hali iliyosababisha kupandishwa ndege na kurudishwa tena huko kendelea na matibabu.

Kabla ya kurudishwa Sauzi, katika video iliyosambaa juzi ilimwonyesha Dimpoz akiwatakia Waislam Idd El Haji njema na kusema kwa sasa hali yake anaendelea ku-recover.

Imeelezwa kwamba, Gavana wa Mombasa, Hassan Joho ndiye amekuwa msatari wa mbele kumsaidia Dimpoz katika matibabu yake baada ya kumgundua kuwa ana tatizo katika koo wakati wa harusi ya Alikiba iliyofanyika Mombasa miezi michache iliyopita.

Joho alichukua jukumu la kumpeleka kwa daktari wake na baada kufanyiwa vipimo vya awali na kugundua tatizo hilo, alipelekwa Sauzi kufanyiwa vipimo zaidi, matibabu na upasuaji.

Hata hivyo Watanzania na mashabiki wake walioguswa na tatizo hilo, wamekuwa wakijitoa kuchangia chochote na kumuombea msanii huyo apone ili arejee kujiunga nasi ktk ujenzi wa Taifa letu Tanzania.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items