Roma awafungukia Basata kuwa inaua sanaa


MKALI wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki ameamua kuwachana Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) huku akidai kuwa taasisi hiyo inaua sanaa, ubunifu na vipaji vya Watanzania.

Roma amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kuwaomba Watanzania waeleze makosa yanayopatikana kwenye wimbo wake mpya aliyoimba na rapa mwenzake na Stamina  uitwao Parapanda.


Jana, Jumatatu, Agosti 6, 2018 Roma na Stamina waliitwa BASATA ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa wa taasisi hiyo alisema waliwaita ili kuwaelekeza kuhusu sheria na kanuni mpya za Baraza hilo.


Mpya zaidi Nzee zaidi