Viongozi wa watano wa chama kikuu cha ushirika mkoani Kilimanjaro KNCU wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi zaidi ya shilingi bilioni 4.9 wameendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.
Viongozi hao ambao wamerejeshwa rumande ni aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro KNCU Aloyce Kitau,,Makamu Mwenyekiti wa KNCU Hatibu Mwanga na Meneja Mkuu WA KNCU Honest Temba,
Wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda cha kukoboa KAHAWA TCCO Meynard Swai na Meneja wake Andre Kleruu.
Aidha mawakili upande wa utetezi wamewakilisha ombi lakubadilishwa siku ya Jumanne iliyopangwa kusikiliza kesi hiyo kwa Hakimu Mkazi Moshi Bernazitha Maziku kutokana na wingi wa mahabusu pamoja afya za viongozi hao kudhoofu.
Hata hivyo Hakimu Mkazi-Moshi Bernazitha Maziku ameridhia ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 22,mwaka huu.
