Waziri Kalemani atoa onyo kwa viongozi wa TANESCO


Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani amesitisha uagizaji wa nyaya za kusambaza na kuwaunganishia wateja umeme toka nje ya nchi kuanzia leo na kuahidi kuwachukulia hatua viongozi wa Shirika la umeme nchi pamoja na wakala wa usambazaji umeme vijijini-REA-watakaoshindwa kuwachukulia hatua makandarasi wanaokiuka agizo hilo.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea viwanda vinavyotengeneza vifaa vya umeme nchini ili kujionea uwezo wa viwanda hivyo, Dk Kalemani amesema wananchi wanashindwa kuunganishiwa umeme ndani ya siku saba kutokana na visingizo vya uagizaji ya nyaya toka nje ya nchi wakati viwanda vilivyo nchni vinauwezo mkubwa wa kutengeneza nyaya hizo kwa haraka zaidi.

Aidha Dk Kalemani ameagiza makampuni yote yanayotengeneza vifaa vya umeme nchini kutengeneza vifaa vyenye ubora na kwa bei nafuu ili kiliwezesha Shirika la umeme kulipa madeni yake kutokana na idadi kubwa ya madeni yanasababishwa na ununuzi wa vifaa kwa bei kubwa.
Mpya zaidi Nzee zaidi