BARAZA LA ARDHI LASITISHA UJENZI WA NYUMBA
Na Ferdinand Shayo,Kilimanjaro .
Baraza la Ardhi la Kijiji cha Kisale kata ya Kisale Msaranga Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro limesitisha ujenzi wa nyumba katika kiwanja cha vijana wawili wenye ulemavu wa macho,miguu na akili baada ya kuuzwa visivyo halali na baba yao mzazi ambaye anatuhumiwa kwa ulevi wa kupindukia.
Katibu wa Baraza hilo John Tarimo amesema, hatua hiyo imechukuliwa baada ya serikali ya kijiji kupokea malalamiko kutoka kwa familia ya vijana hao juu ya uuzwaji wa kiwanja hicho chenye ukubwa wa wastani wa robo Ekari.
Tarimo amesema kuwa , baraza hilo baada ya kuridhika na maelezo ya upande wa familia imesitisha ujenzi wa nyumba hiyo ya bi katerina valeri mpaka baraza la ardhi la kata ya kisale msaranga litakapoipitia hukumu ya baraza la ardhi la kijiji hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Familia hiyo Bw .William Massawe amesema, baba mzazi wa vijana hao bw adabu mtaranyia amekuwa akiuza ardhi yake ya wastani wa ekari mbili kwa watu tofauti na kubakiza robo ekari bila kujali maslahi ya baadae ya watoto wake hao dionisi mtaranyia na severini mtaranyia .
Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw Joseph Mtui amesema,familia hiyo ilipeleka malalamiko hayo baada ya kuona ujenzi ukianza katika kiwanja hicho na kulipeleka suala hilo kwenye baraza la ardhi la kijiji kwa uamuzi kwa kuwa vijana hao wanaishi katika mazingira magumu na bibi yao mwenye wa umri wa miaka 88 .
Baba Mzazi wa vijana hao Bw Adabu Mtaranyia amekiri kuuza kiwanja hicho kwa shs. 2mil/= kwa bi katerina valeri kwa madai ya kutaka kuwahudumia vijana wake madai ambayo yalipingwa vikali na wanafamilia.