Kauli ya Petit Man baada ya kuambiwa amempachika mimba mwanamke mwingine

Mume wa dada wa Diamond Esma Platinumz, Petit Man afunguka kwa mara ya kwanza baada ya kusambaa kwa sauti zinazodhaniwa kuwa ni za kwake akizungumza na mwanadada anaedaiwa kuwa ni mpenzi wake.

Akiongea na U Heard, Petit alidai yeye anashida na watoto kwahiyo kama kuna mwanamke ambaye anadai anamtoto wake basi ajitokeze.

“Azae tu sisi hatukataagi watoto,” alisema Petit baada ya kuambiwa kuna mwanamke Mnyarwanda ana mimba yake.

Aliongeza,”Watoto kwangu ni baraka kweli kweli, kwa sasa nina mtoto mmoja tu, nahitaji waongezeke familia iwe kubwa zaidi, kwahiyo yeye kama ana kibendi changu azae huu sio muda wa maneno,”

Mapema leo asubuhi Mange alikuwa kwenye malumbano na mke wa Petit, Esma na ndipo mwanadada huyo ambaye anaishi Marekani akaamua kuvujisha sauti hizo ambazo anasikika Petit akimbembeleza Mnyarwanda huyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia