Na.Thabit madai,Zanzibar.
Mkoa wa Mjini Magharibi umepata wawakilishi wake wa mchezo wa Mpira wa Kikapu watakaowakilisha Mkoa huo kwenye Mashindano ya Mchezo wa kikapu kwa ngazi ya Taifa yatakayoanza kutuma vumbi September 18 hadi 23 mwaka huu ambapo kilele chake kitafanyika uwanja wa Amani.
Mashindano hayo hujulikana kama mashindano ya Elimu Bila malipo hufanyika kila mwaka na kujumuisha skuli zote Zanzibar.
Timu zilizopata nafasi kwa mwaka huu kwenda kwenye Mashindano ya Taifa ya Elimu Bila ya Malipo kutoka Mkoa huo kwa upande wa Sekondari ni Skuli ya Haile Salas Wanaume na Regeza Mwendo Wanawake ambapo kwa Msingi ni Skuli ya Kijichi kwa Wanaume na Shauri Moyo kwa Wanawake.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi mhe, Ayoub Mohammed Mahmoud aliwataka walimu kujua wajibu wao wa kuhakikisha wanafunzi wanapatiwa haki yao ya msingi ya kushiriki katika mchezo ambapo inafaida nyingi kwao.
Alisema Michezo ni sehemu muhimu kwenye Elimu huku akiwapa hamasa timu hizo kuwaandalia zawadi nono watakapochukua Ubingwa kwenye Mashindano ya Elimu Bila ya Malipo ya Taifa kwa kuuwakilisha vyema Mkoa huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Michezo na Utamaduni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amaali Zanzibar amesema mafanikio na hamasa ya Mashindano hayo ni matunda ya kuwepo mpango wa sports 55 ambao umebuniwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
Michezo ya kikapu katika mashindano hayo hufanyika katika kiwanja cha maisara mjini magharib unguja.