Maimartha aingilia kati sakata la Wema na Mobeto


Kwenye Mitandao ya Kijamii baada ya kuwa na mjadala kuhusu nani anayependwa na kukubalika zaidi Tanzania kati ya Wema Sepetu na Mwanamitindo Hamisa Mobeto, Mtangazaji maarufu Tanzania, Maimartha Jesse ‘Mai’ amefunguka kuhusu sakata hilo.

Akipiga stori na moja ya Chombo cha habari nchini Mai alisema hakuna na hatatokea mrembo mwingine anayependwa na kukubalika kama Wema hivyo wanaompigia debe Mobeto kwamba ndiye anayekubalika sana kwa sasa wanajisumbua tu.

“Wema ndiye Tanzania Sweetheart, hakuna wa kufanana naye na hatatokea mwingine kama yeye, hii ni namba nyingine, wanaosema Mobeto anamzidi ni waongo na hawajafanya tathmini zao vizuri, Wema anapendwa na kila mtu kuanzia watoto hadi wazee,” alisema Mai.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia