Mbowe kutoa sababu za Chadema kushindwa Monduli na Ukonga


Baada ya kumalizika kwa uchaguzi mdogo uliofanyika juzi jumapili ya Septemba 16 na kushindwa kutetea viti vyake viwili vya ubunge ilivyokuwa ikivitetea, Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kinatarajia kuibuka kesho na majibu ya kushindwa kwake.

Uchaguzi huo ulifanyika kwenye baadhi ya kata nchini na majimbo mawili ya Ukonga na Monduli ambapo kote huko wagombea wa CCM Julius Kalanga na Mwita Waitara ambao walitokea Chadema walifanikiwa kuibuka na ushindi.

Chadema wamesema watatoa msimamo wao kuhusiana na uchaguzi huo na hatua ambazo wanatarajia kuchukua.

Kamati Kuu ya Chama hicho kupitia kwa Mwenyekiti wake Taifa, Freeman Mbowe ilikaa ndani kwa siku kadhaa tangu kumalizika kwa uchaguzi huo na kesho watatoa tathimini na msimamo wao juu ya masuala mbalimbali.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items