Polisi waonywa kutokujihusisha na vitendo vya rushwa


Na Paschal D.Lucas,Mwanza.

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limetoa onyo kali kwa askari wake na raia kwa ujumla kwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kuwataka askari kufanya kazi kwa waledi na kuacha kuwabambikizia kesi watu wasio na makosa kwa kuwaweka mahabusu kwenye vituo vya polisi.

Hayo yametolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi Jonathan Shanna wakati akizungumza na maofisa  wa ukaguzi na askari wenye vyeo mbalimbali wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika katika Bwalo la Polisi Mabatini jijini humo.

Kamanda Shanna amekemea tabia ya baadhi ya askari kuomba na kupokea rushwa huku akiwanyoshea vidole raia wanaowashawishi kwa kutoa rushwa huku akiongeza kuwa mikakati mathubuti imewekwa ambapo atakayebainika kujihuusisha na vitendo hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Ameongeza kuwa atakagua mahabusu zote zilizopo katika vituo vya polisi mkoani humo ili kubaini kama kuna watu wamebambikiwa kesi ili achukue hatua stahiki za kisheria.

Aidha katika hatua nyingine ametangaza kufanya msako mkali dhidi ya  Waganga wa jadi wanaojihusisha na upigaji ramli chonganishi zinazopelekea mauaji yatokanayo na imani za kishirikina.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items