Queen Darleen afunguka hajawahi kushuka kimuziki


Queen Darleen ambaye ni Msanii wa muziki nchini Tanzania, amesema kuwa yeye kwenye muziki wake hajawahi kushuka kama watu wengi wanavyodai kuwa Wasanii wakike wanashindwa ku-maintain kwenye game.

Darleen amesema kuwa yeye hajawahi kushuka toka enzi hizo na kujifananisha na marehemu Bi. Kidude kuwa Uzee wake utaendelea kuwa mzuri hata kama umri wake ukiendelea kumtupa mkono.

“Mimi sijui wao lakini mimi toka  hizo zama za kina Lady Jaydee, akina Ray C mpaka leo hii mimi bado nipo, nakwenda nao level za akina Nandy, yaani mimi nipo humo humo na sitoki yaani na wasitegee kutoka leo, kesho yaani mimi kama bi Kidude nakufa na muziki wangu,“amesema Queen Darleen kwenye mahojiano yake na Wasafi TV.

Pia Queen Darleen amezungumzia mavazi yake ambayo mashabiki wake wamekuwa wakimshambulia kuwa anavaa nusu utupu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Mtanzania.

“Kama mimi navaa najiona mwenyewe napendeza, niko fresh, lakini mtu anakuja anakwambia unavyovaa umevaa vibaya hujapendeza? My Friend pesa yangu ambayo nimenunulia nguo mimi unayoniambia sijapendeza, hiyo simu yako uliyoshika gharama yake hazilingani.. Tusipangiane mavazi wala maisha.“amesema Queen Darleeen.

Hata hivyo Queen Darleen ameahidi kuachia kazi yake mpya ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa na amewataka mashabiki wake wawe wavumilivu kwani WCB kuna mfumo wa namna ya kuachia ngoma.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia