WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Riziki Pembe Juma, amewataka wanaume wanaoshindwa kujizuia na matamanio yao bora waoe kuliko kuwabaka watoto wadogo.
Alisema kuwa licha ya serikali kutunga sheria mbalimbali za kudhibiti udhalilishaji wa kijinsia, lakini bado matukio hayo yamekuwa yakiendelea Zanzibar.
Akizungumza jana katika mkutano wa wazi wa kutoa maoni jinsi ya kuondokana na vitendo hivyo, viwanja vya Jamhuri Kariakoo, alisema kuwa ushirikiano wa pamoja ndiyo unaohitajika lakini kuiachia serikali pekee jambo hilo haliwezi kuondoka.
Alisema kuwa anaumia kusikia kila siku wanafunzi wa shule wanadhalilishwa, kwani hali hiyo haipendezi, inachukiza na ni aibu kubwa hasa kwa Zanzibar.
“Sote tunaguswa na tunaumizwa mimi binafsi nikiwa waziri wa kusimamia elimu ndani ya Zanzibar hii, nina wanafunzi ambao ndio watoto wetu wote ambao nawasimamia, lakini inaniumiza kusikia wanadhalilishwa, ni fedheha, aibu, kashfa na uchafu tuseme imetosha na iwe basi,” alisema.
Aidha, waziri huyo alisema wizara tayari imemsimamisha kazi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kinuni kwa tuhuma za kutaka kumlawiti mtoto ili kupisha uchunguzi.
Kwa upande wao, wananchi walioshiriki katika mkutano huo wa wazi, walisema kuwa ili vitendo hivyo viweze kuondoka serikali itoe adhabu kali kwa watuhumiwa pamoja na kupambana na rushwa katika vyombo vya sheria.
Akizungumza katika mkutano huo wa wananchi, Kheir Miraji Othman, alisema kuwa washtakiwa wa matendo ya udhalilishaji wapigwe viboko hadharani na wafungwe jela maisha.
Alisema kuwa adhabu madhubuti ni kutoa hukumu muda mfupi baada ya tukio kufanyika na siyo kutolewa baada ya miaka miwili tangu tukio lifanyike.
Mwananchi mwingine, Maimuna Adam Ferudhi, alisema kuwa wakati umefika sasa kuruhusiwa wananchi kuchukua hatua mikononi mwao kwa watuhumiwa wa matukio ya udhalilishaji wa kijinsia.
Alisema wameshachoka kupeleka kesi katika vyombo vya sheria kwani wanaona kuwa haki haitendeki na badala wanaishia kuona watuhumiwa wakiwa mitaani wanaendelea na shughuli zao bila ya kuchukuliwa hatua.
“Kama serikali inataka kweli matukio haya yasiwepo hebu watuachie sisi wananchi tuchukue sheria mikononi mwetu kwa hawa watuhumiwa…mimi binafsi nikibakiwa mtoto wangu siachi mtu,” alisema.
Mkutano huo wa wazi uliowashirikisha wananchi mbalimbali umeandaliwa na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto kutokana na kushamiri kwa matukio ya udhalilishaji wa kijinsia.