SAID Mbonde (20), mkazi wa Kijiji cha Chapita, Kata ya Mingumbi Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, amekufa kwa kuteketea kwa moto akiwa amelala usingizi ndani ya nyumba yake.
Hayo yameelezwa na Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Haji Limba, alipokuwa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai, alipofika kijijini hapo kuwafariji ndugu na jamaa wa marehemu.
Limba alisema tukio hilo ambalo liliteketeza nyumba tatu za jirani na moja aliyokuwa anaishi marehemu, lilitokea wiki iliyopita.
Limba alisema katika tukio hilo, watu wawili akiwamo Issa Bwango (19) na kibibi kizee ambaye hakumtaja jina, walinusulika kifo kutokana na moto huo, ambao unaodaiwa kuchangiwa na utunzaji usio makini wa mafuta aina ya petroli.
Mtendaji huyo wa kata alieleza kuwa licha ya kupoteza maisha ya mwananchi huyo, moto huo uliteketeza nyumba nyingine tatu na mali mbalimbali, ikiwamo mashine moja ya kusaga nafaka, magodoro, vitanda, vyakula, vyombo vya ndani na nguo, ambavyo hata hivyo, thamani yake haijafahamika.
“Mali zote zilizokuwamo ndani ya nyumba hizo, zimeungua kabisa na hakuna kilichosalia,” alisema Limba.
Limba alisema kwamba petroli inayodaiwa kuwa chanzo, ilikuwa imehifadhiwa kwenye nyumba hiyo aliyokuwa akiishi marehemu Mbonde.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa chanzo cha moto huo ni kumwagika kwa petroli hiyo, wakati Bwango alipokuwa anamimina petroli kutoka kifaa kimoja kwenda kingine, huku akiwa na sigara.
DC Ngubiagai akizungumza wakati wa kuwafariji wafiwa na waathirika hao, alisema amesikitishwa na tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha tabia ya utunzaji holela wa vitu vinavyosababisha milipuko, huku akiwaonya wauza petroli bila kuwa na leseni kuacha mara moja.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kilwa, Dk. Halfan Ilekizemba, alithibitisha kumpokea majeruhi Mbonde, aliyepewa rufani kutoka Kituo cha Afya cha Tingi, na kueleza kuwa aliungua miguu yote na hali yake anaendelea vizuri.