Mabaraza ya madiwani nchini ikiwemo la manispaa ya Ilala wametakiwa kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao ili kuhakikisha hakuna vikwazo vinavyojitokeza katika utekelezaji wa miradi hiyo ambayo tayari serikali imeshatoa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo kwenye maeneo mbalimbali ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI ) Suleiman Jafo alipotembelea baadhi ya miradi ikiwemo ya ujenzi wa machinjio ya kisasa Vingunguti ,ujenzi wa kituo kipya cha afya Kivule na upanuzi wa majengo ya afya ya kituo cha Buguruni kwa Mnyamani na kuonesha hali ya kutokuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.
