Msanii kutokea WCB, Harmonize amesema ni furaha kubwa kuona wimbo waliofanya na Professor Jay umetoka na ni hesimu kubwa amepewa na msanii huyo mkongwe.
Harmonize ameeleza kuwa Pofessor Jay ni msanii mkubwa na pia kiongozi mwenye ushawishi kwenye jamii hivyo kufanya naye kazi ni rafaja kwake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ameandika;
"Weka mbali kuwa wewe ni mwanamuziki uliyefanya makubwa sana katika hilo Taifa lakini pia serikali pamoja na wananchi wasiohesabika wameweka imani yao pamoja na kukukabidhi jimbo la Mikumi hii ni bahati na heshima iliyoje kuapata nafasi ya kushiriki katika kazi yako kaka Professor Jay," ameeleza Harmonize.
Harmonize atakuwa msanii wa pili kutokea WCB kufanya wimbo na Professor Jay baada ya Diamond Platnumz ambaye alishirikishwa na rapper huyo katika wimbo uitwao Kipi Sijasikia ambao ulitoka mwaka 2014 .
Wimbo huo ulikuwa wenye mafanikio makubwa ambapo mwaka 2015 ulishinda tuzo kupitia Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kama wimbo bora wa Hip Hop.