Na John Walter-Manyara
Asilimia Themanini [80%] ya wagonjwa wanaotibiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Manyara wanaugua magonjwa yatokanayo na Uchafu.
Kwa mujibu wa afisa afya na Mazingira mkoa wa Manyara Evance Dabrick Semkoko meyataja magonjwa hayo kuwa ni, Macho,Masikio,Meno,Kuharisha,homa ya matumbo,Kutapika,Kipindu Pindu,U.T.I,Magonjwa ya ngozi na mengine yanayohusisha uchafu wa mtu binafsi na mazingira ambayo yanasababisha wananchi kutumia fedha nyingi katika kuyatibu badala ya kufanya shughuli za maendeleo.
Akizungumza na kituo hiki ofisini kwake amesema, Jumla ya Wagojwa waliohudhuria kliniki za nje [OPD] kwa mwezi Novemba mwaka huu pekee kwa Manyara ni laki saba kwa magonjwa yote ambapo ilipatikana asilimia 10% ya wagonjwa wanaoharisha,idadi ambayo ukijumlisha na magojwa mengine yanayotokana na uchafu unapata asilimia zaidi ya 80%.
Aidha amesema serikali ya awamu ya tano inakabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto lakini kwa mwenendo wa wananchi wengi inakuwa ni vigumu kuweza kukabili hilo kutokana na wengi kushindwa kuzingatia hatua za kunawa mikono.
Semkoko amesema hali hiyo inasababishwa kwa kiwango kikubwa na kukosa vyoo bora,kujisaidia vichakani,upatikanaji wa shida kwa huduma za maji,,uchumi,kijamii,makuzi ya watoto,mila na desturi pamoja na tamaduni za watu.
Mkoa wa Manyara na Tanzania kwa ujumla unakabiliwa na tatizo kubwa ya suala la uchafu ambao unapelekea wananchi na jamii kwa ujuma kupata matatizo mengi ya kiafya inayowalazimu wengi kukimbia katika vituo vya afya kupata matibabu ambapo wanatumia gharama kubwa.
Suala la Usafi ni suala la msingi sana na ambalo kama mkoa sisi tumeliweka kama kipaumbele ambalo linaweza kutuletea maendeleo katika Nyanja zote,na kwa sababu tumeweka katika mikakati tunatekeleza kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira ambayo imetusaidia sana katika kuongeza idadi ya kaya Mkoa wa Manyara zenye vyoo bora.
Mkoa wa manyara ulianza na idadi ya vyoo asilimia 36% mwaka 2016 ambapo mpaka mwaka 2017-2018 imefanikiwa kuwa na vyoo kwa asilimia 60% na kuhamasisha watu kuwa na vibuyu chirizi pindi wanaponawa mikono kwa kufuata hatua kumi muhimu baada na kabla ya kula au kutoka chooni.
