Diamond aachia nyimbo 7 kutoka kwenye albamu yake


Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz ameachia nyimbo saba kutoka kwenye albamu yake ya A Boy From Tandale.

Hizi ni nyimbo ambazo zilikuwa hazijatoka zaidi kuuzwa kwenye mitandao kama Spotify na iTunes ila sasa zinapatikana kwenye channel yake ya YouTube.

Nyimbo zilizoachiwa ni kama Fay Away ambazo amemshirikisha Vanessa Mdee, Pamela ambayo pia amemshirikisha Young Killer, Amanda aliyoshirikiana na Jah Prayzay, nyimbo nyingine ni kama Baikoko, Kosa Langu, Nikuone na Sijaona.

Albanu hiyo yenye nyimbo zipatazo 18 uzinduzi wake ulifanyika March 14, 2018 nchini Kenya na baada ya hapo alifanya tour ya mwezi mzima nchini Marekani kwa ajili ya albamu hiyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items