IGP Sirro aeleza gari lililohusika utekaji wa Mo Dewji


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Simon Sirro amesema polisi nchini wamepata maelezo muhimu kuhusu gari lililotumiwa na watu waliomteka mfanyabiashara Mo Dewji.

Amesema gari hilo ambalo muundo wake ni Toyota Surf na yenye rangi ya bluu nyeusi, na lenye ufito wa rangi ya shaba kwa chini lilitokea nchi jirani ambayo hakuitaja na kueleza kuwa liliingia nchini Tanzania mnamo Septemba 1, amewaonesha wanahabari picha za gari hilo ambapo amesema wanaomba maelezo zaidi.

Kamanda Sirro amesema wanafuatilia kwa pamoja na polisi wa kimataifa wa Interpol.

Amesema kufikia sasa hawafahamu iwapo gari hilo, ambalo wamebaini nambari yake ya usajili ni AGX 404 MC, bado lipo Tanzania na akawaomba wananchi kutoa taarifa kwa polisi wakiliona.

"Tumefuatilia na watu wetu wamekwenda mpaka mpakani na wameweza kuona lilipita 1 Septemba 2018. Tumepata maelezo ya kutosha ambayo siwezi kuyasema," amesema.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items