Profesa Lipumba na Maalim Seif kuunganisha nguvu pamoja?


Chama Cha Wananchi CUF upande wa Maalim Seif Sharif Hamad kupitia Kwa Kaimu Mkurugenzi wa habari, Mbarara Maharagande umesema Chama hicho kinatarajiwa kukaa kikao cha kamati ya utendaji kwa ajili kutoa maamuzi kama watashirikiana tena na Profesa Lipumba katika uchaguzi wa marudio Ukerewe.

Maharagande amesema “tutakuwa na kikao wiki inayokuja na tutatoa maamuzi kama tutashirikiana na upande wa Lipumba kwenye uchaguzi wa marudio katika majimbo yanayorudia uchaguzi Tanzania bara.” amesema Maharagande.

Katika Uchaguzi wa marudio uliofanyika Jimbo la Liwale pande zote mbili ziliungana kumnadi aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia CUF, Mohamed Mtesa.

Aidha uongozi wa chama hicho upande wa Maalim Seif umesema haujaona jambo lolote la kujifunza juu ya kumaliza migogoro wao na Profesa Lipumba kama ilivyokuwa kupitia mgogoro wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA uliohusisha wabunge wake wawili, Saed Kubenea wa Ubungo na Mbunge wa Moshi Vijijini, Athony Komu.

Maharagande amesema “tatizo limetokea na wameitana, matatizo yao hayafanani na ya kwetu yale yako ndani yao, sisi kwetu kuna mkono wa dola kupitia Profesa Lipumba ili kuharibu Chama Cha wananchi CUF.”
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items