Serikali yaombwa kuwachukulia hatua kali Wazazi wanaokeketa watoto wa kike


Serikali imeombwa kuwachukulia hatua kali wazazi na walezi Wilayani Tarime Mkoani Mara ambao wanakubali kukeketa watoto wa kike ambao ukimbia ukeketaji kipindi hicho na baada ya zoezi kumalizika mabinti hao waliokimbia ukamatwa na kukeketwa hivyo wameiomba serikali kuendelea kusimamia vikali sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ili kutokomeza suala la ukeketaji kwa mtoto wa kike huku baadhi yao wakikeketwa usiku.

Hayo yamebainisha na baadhi ya wazazi katika kata ya Pemba kipindi wakipatiwa elimu ya kupinga Ukeketaji kupitia Shirika la Tanzania Mindset Network chini ya Ufadhili wa TGNP Mtandao kupitia Shirika la Idadi ya Watu Ulimwenguni UNFPA.

Wazazi hao wamedai kuwa kipindi cha ukeketaji watoto wamekuwakikimbia ili wasikeketwa mpaka msimu wa ukeketaji unamalizika lakini pale wanarudi kijijijini ukamatwa na jamii na kukeketwa kwa Nguvu hivyo wameomba serikali kuwachukulia hatua kali wazazi na walezi watakaoshiriki katika kitendo hicho.

“Pia wazazi hao wamesema kuwa kuna tetesi za watoto wa kike kukeketwa nyakati za usiku baada ya serikali kwa kushirikiana na mashiriki kupinga vikali ukeketaji.Kuna Ngariba tunamfaamu yuko maeneo ya mbali ameibuka hivi karibuni tunajua atakeketa watoto wetu usiku hivyo sasa serikali itambue suala hilo” alisema Mmoja wa wazazi katika kijiji cha Nyabisaga kata ya Pemba.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items