TANZIA: Muigizaji Ramadhan Mrisho ‘Mashaka’ amefariki Dunia

Aliyewahi kuwa muigizaji wa kundi la sanaa la Kaole, Ramadhan Mrisho Ditopile maarufu kama Mashaka amefariki dunia katika hospitali ya Amana iliyopo Ilala ,Dar Es Salaam  asubuhi ya leo October 20,2018.

Mpaka sasa bado haujatajwa ugonjwa uliosababisha kifo cha Ramadhan Mrisho ‘Mashaka’ ingawa inaelezwa kuwa Marehemu alionekana kuzidiwa jana usiku na hivyo kukumbizwa hospitali na ndipo umauti ulipomkuta katika hospitali ya Amana.

Marehemu Mashaka aliwahi kuigiza na kuonekana kwenye maigizo mbalimbali ya Kaole yaliyotamba mwanzoni mwa miaka ya 2000..
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items