TUNAANZA UPYA!! Lulu kurudi kivingine kwenye Filamu

Msanii wa Elizabeth Michael ‘Lulu’ yupo locationi kwa ajili ya kuandaa movie mpya.

Aliyefichua hilo ni mchumba wa Lulu, Majizzo ambaye amechapisha picha ya Lulu kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika jumbe unaosomeka; 'Back to business @elizabethmichaelofficial'

Kwanini karudi  upya?

Novemba 13, 2017 muigizaji wa filamu Bongo, Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua aliyekuwa muigizaji mwenzake Steven Kanumba bila kukusudia.

Utakumbuka kifo cha Kanumba kilitokea April 04, 2012 na mwaka huo alifunguliwa mashkata na hukumu ikaja kutoka 2017.

Usiku wa May 13, 2018 ziliaza kusambaa taarifa mtandaoni kuwa Lulu yupo uraia, siku iliyofuata mamlaka husika zilidhibitisha kuwa Lulu ametoka kwa msamaha wa Rais Magufuli. Hivyo baada ya hayo yote Lulu anarejea tena kwenye filamu kwa kufungua ukurasa mpya.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items