VIDEO: ACT - Wazalendo waivaa Serikali sakata la elimu, "huwezi kumkataa mtoto uliyemzaa mwenyewe'


Chama cha ACT Wazalendo kimeduwazwa na hatua ya Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuikataa ripoti yake yenyewe (Annual Education Sector Peformance Report) kwa sababu tu baadhi ya maudhui yake yanaonesha dhahiri kuporomoka kwa kiwango cha wanafunzi wa shule ya msingi  wanaojua kusoma.

Taarifa hiyo imebainishwa leo na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT - Wazalendo Ado Shaibu alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa ripoti ya AESPR inaonesha wazi kwamba kama nchi tumefanya vizuri kiasi katika kuwapeleka watoto shule lakini ni dhahiri kuwa watoto wetu hawajifunzi ipasavyo.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Mpya zaidi Nzee zaidi