Wanawake waongoza kwa matatizo ya macho


Na Paul Mabeja, DODOMA

WANAWAKE walio katika umri wa kati wanetajwa kuwa kundi linaloongoza kwa matatizo ya kuvimba macho kutokana na matumizi ya bidha mbalimbali za urembo.

Bidhaa hizo ni pamoja na Wanja, kupaka rangi machoni pamoja na kubandika kope badindia.

Hayo yalinainishwa jana jijini hapa na kaimu Meneja Mpango wa taifa wa huduma za macho Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk, Bernadetha Shilio, kwenye hafla ya kilele cha siku ya afya ya macho duniani.

Dk, Shilio alisema kuwa matumizi ya bidhaa hizo kwenye macho ya binadamu yanachangia kwa kiasi kikubwa matatizo mbalimbali ya macho.

Alisema takwimu za mwaka jana katika hospitali mbalimbali nchini zinaonyesha kuwa kundi kubwa la wanake walio katika umri wa kati wanaongoza kwa matatizo ya macho kuvimba.

“Wanawake wengi walio katika umri wa kati wamekuwa ndiyo kinara katika tatizo la kuvimba macho ukilinanisha na wale wazee au wanaume hii nikutokana na matumizi ya vipodozi hivyo ambavyo wengi wao wamekuwa wakivitumia katika macho yao”alisema Dk. Shilio.

Aliongeza kuwa matumizi ya vipozi hivyo katika macho yanamweka mtumaji katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya macho kutokana na kemikali ambazo zimetumika katika utengenezaji wake.

“Hatari sana katika kona za jicho mtu kuweka kitu ambacho haeliwi kimetengezwa na kitu gani jicho linapaswa liwe safi ili kuwa na afya njema”alisema.

Aidha aliwataka wanachi kuwa na tabia ya kupima afya ya macho yao angalau mara moja kila mwaka ili waweze kutambua afya zao.

Pia alitoa onyo kwa wanachi kuacha tabia ya kutumia miwani bila kuwaona wataalam wa afya ya macho kwani hali hiyo inaweza kusababisha kuongeza tatizo.

“Hatupaswi kuvaa miwani ya macho bila kuandikiwa na wataalam lakini pia hata matumizi ya dawa tunapaswa kuandikiwa na wataalam na siyo kuweka dawa katika jicho hata ile aliyo andikiwa wenzio hali hii ni hatari sana kwa afya zetu”alisema Dk, Shilio.

Hatahivyo alisema kuwa hadi kufikia jana taarifa kutoka mikoa tisa  watu 5,000 wamefanyiwa uchunguzi na 200 wamefanyiwa upasuaji.

Mwisho