Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani Siasa za kumwaga damu


Na Timothy Itembe Tarime.

CHAMA cha mapinduzi CCM wilaya Tarime mkoani Mara kimelaani baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani kuwa ndiop wanachangia kufanya  siasa za kumwaga damu jambo ambali ni kinyume cha mwenyezi Mungu hata mbele ya sheria za nchi yetu.

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya Tarime mkoani Mara,Daud Ngicho alisema hayo juzi wakati akipokea wanachama wapya wa kata ya Nyanungu ambao walihama  vyama vyao na kujiunga na chama kipya cha CCM.

Akipokea wanachama wapya 44 waliohama vyama vyao na kujiunga na Chama cha mapinduzi CCM Ngicho alisema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanafurahia kufanya siasa za kumwaga Damu jambo ambalo  hakikubaliki kwa jamii na hata mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyekiti huyo alitumia nafasi hiyo kufungua shina la wakereketwa Umoja wa vijana UVCCM kata ya Nyanungu huku akiwachangia shilingi milioni moja kwaajili ya kuanzisha miradi ya maendeleo na kuinua kipato chao ili kuendana na kauli ya Rais wa awamu ya Tano John Pombe Magufuli ya Tanzania ya viwanda.

"Ndugu zangu kwasababu nawapenda watu wa Nyanungu napenda kuwachangia vijana wa umoja wa vijana UVCCM kata ya Nyanungu shilingi milioni moja kwaajili ya kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo na kukuza vipato vyao pia napenda  kuchangia tripu tano za mchanga ujenzi wa Ofisi ya CCM kata ya Nyanungu inayojengwa iliyo katika hatua ya msingi alisema Ngicho.

Mmoja wa wanachama hao wapya Wangoba Mogoyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa Chadema kitongoji cha Kwibate ambaye alikihama chama hicho alisema kuwa yeye na wanachama wengine wamehamia CCM kwasababu Chadema kimepoteza mwelekeo.

Naye katibu wa Chama cha mapinduzi wilaya Tarime,Khamis Mkaruka alisema kuwa Chama chake kimejipanga kuwasajili wanachama wake kwanjia ya Elktroniki ili kuytambulikana kwenye sisitimu na kuwa wanachama wote wanatakiwa kulipia kadi zao Ada ya uwanachama kwa lengo la kuwa hai.

"Tumepokea wanachama wapya 44 ambao wamerudi nyumbani kumenoga wanachama kutoka chama cha ACT Wazalendo ni 05,wafuasi wa chama cha NCCR Mageuzi ni 03,wanachama kutoka Chama cha Chadema 44 huku wanachama kutoka chama cha CUF ni mwanachama mmoja"alisema Mkaruka.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items