Loading...

Nov 9, 2018

Haya ndio mambo walioafikiana TFF na Yanga


Baada ya kuitikia wito wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), uongozi wa klabu ya Yanga umesema kikao walichokaa jana kilienda vizuri.

Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Samuel Lukumay, ameeleza kuwa kikao hicho kilikwenda vizuri huku akiwataka wanayanga watulie.

Katika kikao hicho ambacho kiliwa na lengo la kujadili juu ya hatma ya klabu hiyo kusimamiwa uchaguzi wake na TFF, imewalazimu Yanga kwenda kukaa na Barala za Wadhamini.

Lukumay ameeleza kuwa kutakuwa na kikao kingine kitakachohusisha Baraza la Wadhamini Jumapili ya wiki hii na pengine mambo yatakuwa yamekamilika kwa asilimia 100.

Yanga wamegomea kusimamiwa uchaguzi wao na Kamati ua Uchaguzi ya TFF hivyo imewabidi TFF watumie busara ya kuelewana nao taratibu.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger